Mrembo Ester wa Bongo Movies Adai Marafiki zake ni Wavulana tu..Asema Wanawake ni Masnichi Wakubwa - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Jul 2015

Mrembo Ester wa Bongo Movies Adai Marafiki zake ni Wavulana tu..Asema Wanawake ni Masnichi Wakubwa

MUIGIZAJI mwenye mvuto anayekuja kasi katika tasnia ya filamu Bongo, Ester Kiama ameweka bayana kuwa hapendi kuwa na marafiki wa kike na hana.
Muigizaji mwenye mvuto anayekuja kasi katika tasnia ya filamu Bongo, Ester Kiama.
Akifunguka kiunagaubaga, Ester alisema kutokana na malezi na maisha yalivyo sasa inabidi aepuke marafiki ambao wengi wao ni wanafiki.
“Wengi wanajua naringa sana lakini ukweli sipo hivyo ndiyo maana muda mwingi nautumia katika kufanya shughuli zangu na kujiepusha na makundi kwani najua madhara yake, washikaji zangu ni wanaume kwani najifunza mengi kupitia kwao,” alisema Ester.