Mwigizaji wa Bongo Movies Esha Buheti Akiri Kuchepuka Nje ya Ndoa - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Jul 2015

Mwigizaji wa Bongo Movies Esha Buheti Akiri Kuchepuka Nje ya Ndoa

Mwigizaji Bongo, Esha Buheti, licha ya kuwa ndani ya ndoa, amekiri kuchepuka na mcheza mpira mmoja ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.

Akizungumza na na gazeti la Ijumaa, Esha aliweka wazi hisia zake kuwa kwa sasa ana kifaa kipya chenye hadhi na amekuwa akitupia picha zake mitandaoni kisha anazitoa.

“Najua wambeya watataka kumchunguza mpenzi wangu wa sasa ndiyo maana namuweka mtandaoni kisha nafuta harakaharaka,” alisema Esha.

Esha alifunguka kuwa, pamoja na ‘kidumu’ alichonacho bado yuko kwenye ndoa yake na anamheshimu mumewe aliyezaa naye mtoto mmoja.