Rose Muhando: Nafikiria Kurudi Kwenye Uislamu - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Jul 2015

Rose Muhando: Nafikiria Kurudi Kwenye Uislamu

NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.

Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.

“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.

Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.