CCM wakanusha taarifa inayosambazwa kwa kasi kuhusu Kamati ya Usalama na Maadili - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Jul 2015

CCM wakanusha taarifa inayosambazwa kwa kasi kuhusu Kamati ya Usalama na Maadili


TAARIFA KWA UMMA

Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa na juhudi za uzushi na upotoshaji zinazofanywa na baadhi ya watu kwa malengo binafsi.

CCM inasisitiza kuwa hakuna taarifa yoyote ya Usalama na Maadili iliyoandaliwa na kuchapwa na kwamba kinachosambazwa mtaani ni uzushi wenye lengo la kuwachafua baadhi ya wanaoomba ridhaa ya CCM kuwania nafasi ya Urais kwa malengo mabaya.

CCM haitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote watakaobainika kuendesha harakati za kuandaa na kusambaza uzushi wa aina yoyote dhidi ya shughuli za Chama.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Umma - CCM HQ