BREAKING NEWS....Emmanuel Mbasha Aachiwa Huru Mahakama yaona Hana Hatia ya Kesi ya Ubakaji wa Mdogo wake Flora Mbasha - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Sept 2015

BREAKING NEWS....Emmanuel Mbasha Aachiwa Huru Mahakama yaona Hana Hatia ya Kesi ya Ubakaji wa Mdogo wake Flora Mbasha

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo imemuachia huru mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kosa la ubakaji baada ya kuona hana hatia juu ya madai hayo.
Mbasha alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.

Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutolewa, Mbasha alipiga magoti mbele za watu na kumshukuru Mungu huku akitokwa na machozi ya furaha.