CCM Kwa Sasa inakuwa ni Aibu Kugombania na Ukawa Sera na Zilizowashinda Miaka 53 ya Uhuru. - MULO ENTERTAINER

Latest

1 Sept 2015

CCM Kwa Sasa inakuwa ni Aibu Kugombania na Ukawa Sera na Zilizowashinda Miaka 53 ya Uhuru.

Unapomuona waziri wa uchukuzi akijibu Sera za UKAWA mtu makini anajiuliza maswali mengi sana. Kama mnampango wa kuboresha reli ya kati iweje isiboreshwe miaka 10 ya awamu ya 4?, Air Tanzania imepitia kipindi kigumu miaka 15 sasa mpaka kufikia kuwa shirika lisilo na tija kwa taifa alafu mnasema mnampango na ni sera yenu chama tawala nadhani pengine hii itakuwa akili ya kizee. UKAWA wana wajibu wa kurekebisha yale mlioshindwa katika awamu zote mlizoshikilia dola na kulala tu, Ukawa wanahaki kutumia udhaifu huo kama Kempeni dhidi yenu. Na kwa sasa inakuwa ni aibu kugombania sera zilizowashinda miaka 53 ya uhuru.