Mgombea Mwenza wa CCM Aendelea Kukiuka Taratibu..Wema Sepetu Nae Aaibika Mgahawani - MULO ENTERTAINER

Latest

22 Sept 2015

Mgombea Mwenza wa CCM Aendelea Kukiuka Taratibu..Wema Sepetu Nae Aaibika Mgahawani

Katika hali ya kushangaza mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM mama Samia Suluhu Hassan leo amechelewa kumaliza mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Usagara jijini Tanga.mama Samia alichelewa kufika mkutanoni,a lifika saa 12 kasoro na kuanza kuhutubia saa 12 kamili na kumaliza saa 12 na dakika 40.kwa mujibu wa taratibu mgombea anatakiwa kumaliza mkutano saa 12 kamili lkn taratibu ziliendelea kukanyagwa kanyagwa.

Wakati huo huo mpambe na mpiga debe wa CCM msanii Wema Sepetu amekutana na aibu alipoingia kwenye mgahawa uliipo mjini aliposema CCM oyee watu wote walikaa kimya. Alitamka mabadiliko watu wote kwa pamoja walimjibu Lowassa,baada ya kuzidiwa ndio aliposema eti huyo Lowassa mgonjwa. Kijana mmoja mpenda mabadiliko alimjibu hata raisi kikwete ni mgonjwa ndo maana alikwenda Marekani kufanyiwa operation ya tezi dume. Alipokutana na ugumu huo aliamua kuondoka zake huku akiwa hana la kusema.
CCM wanaamini Tanga ni ngome yao lkn hali imebadilika Tanga ya leo si ile ya 1995.