Picha: Mahujaji 717 Wapoteza Maisha Mecca Baada ya Kukanyagana - MULO ENTERTAINER

Latest

24 Sept 2015

Picha: Mahujaji 717 Wapoteza Maisha Mecca Baada ya Kukanyagana

Takriban mahujaji 717 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana karibu na mji mtakatifu wa kiislam, Mecca nchini Saudi Arabia.
2CB55A5B00000578-3247269-image-m-48_1443093895904
Watu wengine 863 wamejeruhiwa kwenye tukio hilo lililotokea kwenye eneo la Mina, wakati ambapo mahujaji milioni mbili kutoka nchi mbalimbali duniani walikuwa kwenye siku ya mwisho ya Hijja.
2CB7FEC600000578-3247269-image-a-34_1443106902688
Hilo ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha Hijja katika kipindi cha miaka 25.
2CB615B800000578-3247269-image-m-84_1443102599905
Wakati wa Hijja, mahujaji walisafiri kwenda Mina, bonde kubwa lililopo kilomita tano kutoka Mecca, ili kwenda kurusha mawe saba kwenye nguzo za Jamarat.
2CB67BC400000578-3247269-image-a-39_1443107078688
Nguzo hizo zinaaminika kuwa sehemu ambayo shetani alimrubuni Nabii Ibrahiym.
2CB61F7300000578-3247269-image-a-93_1443103462347
Tukio hilo limetokea wiki chache tuu baada ya watu 109 kupoteza maisha baada ya kuanguliwa na cranes kwenye msikiti mkuu wa Mecca.