Baada ya Tanzania Kufungwa 7 Bila na Algeria..Shaffih Dauda Aichana Vibaya TFF, Adai Walikuwa Wanafanya Jitihada za Uongo Kuhadaa Watanzania - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Nov 2015

Baada ya Tanzania Kufungwa 7 Bila na Algeria..Shaffih Dauda Aichana Vibaya TFF, Adai Walikuwa Wanafanya Jitihada za Uongo Kuhadaa Watanzania

From The Desk Of Shaffih Dauda:
Moja kati ya matatizo makubwa ya sisi watanzania ni kutokukubali pale ambapo kuna mtu amekuzidi. Mara nyingi huwa tunadharau yule ana nini, mfano mtu ana gali zuri watasema yule kahongwa au kaiba. Hatukubali uhalisia au mafanikio ya mtu ili kujipa changamoto angalau kama sikufikia au kukaribia mafanikio ya aliyekutangulia.

Maana yake ni kwamba zile jitihada za uhongo zilizokua zifanywa na TFF kuwaaminisha watanzania kwamba tunaweza kuifunga Algeria kitu ambacho ni cha uongo kabisa. Ndio maana mimi toka mwanzoni nilikua napinga kwa asilimia zaidi ya 100 kuhusu swala la kuifunga Algeria. Ndio maana tangu mwanzoni nilitoa ahadi kwamba kama Algeria ikitolewa na Tanzania basi nitaenda gerezani, napapenda uraiani ndio maana nilikua na uhakika hilo swala lisingewezekana.

Mpira hauna short cut ni mipango ambayo ipo clear, TFF ilicheza na saikolojia ya watu baada ya wao kushindwa kazi yao ya msingi kusimamia uwekezaji wa soccer. Waliwadharau Algeria, wakaunda kamati ambazo ilikuwa ni njia ya kuwaada na kuwaaminisha watanzania kwamba inawezekana kirahisi kuwafunga Algeria.

Sifurahii matokeo lakini kwa upande mwingine nafurahia. Hii iwe fundisho kwa viongozi ambao wana mentality za kishabiki badala ya kusimamia na kutengeneza misingi thabiti ya kuendeleza soccer letu, wanabaki kuendeleza propaganda za kuwarubuni watanzania.
Shaffih K. Dauda