Waziri Mkuu wa Serekali ya Awamu ya Tano ni Huyu Hapa - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Nov 2015

Waziri Mkuu wa Serekali ya Awamu ya Tano ni Huyu Hapa

Fumbo kuhusiana na mtu mwenye sifa za kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli limeanza kufumbuliwa.

Hali hiyo inatokana na kile alichokidhihirisha Magufuli siku moja baada ya kuapishwa kwake na pia baada ya hapo wakati alipochukua maamuzi kadhaa ya vitendo, ikiwamo kutoa maelekezo muhimu yaliyodhihirisha aina ya Waziri Mkuu atakayemteua.Kwa mujibu wa muundo wa serikali, Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, ambaye mbali ya kuwa kinara wa mawaziri wengine, ndiye anayetakiwa pia kutoa maamuzi mazito linapojitokeza jambo linalomlazimu kufanya hivyo.

Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya siasa na uongozi nchini wamesema hatua alizochukua Magufuli kuanzia siku ya kwanza ya kuapishwa kwake zinatoa picha ya wazi aina ya watu atakaotaka kuwa nao katika serikali yake.

Baada ya kuapishwa Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Dk. Magufuli alianza kazi siku hiyo hiyo kwa kutoa hotuba iliyosisitiza juu ya kauli mbiu yake ya ‘hapa kazi tu’ katika kutumikia wananchi, kuwafariji waliokuwa wapinzani wake katika urais huku akiwasihi waungane naye kuijenga Tanzania imara na pia alimteua Mwanasheria Mkuu, George Masaju, huku pia akitangaza siku ya kuanza Bunge kuwa ni Novemba 17.

“Ratiba yake katika siku ya kwanza aliyoapishwa ilikuwa ngumu kutokana na wageni wengi waliomtembelea lakini bado hakutaka kuchelewa katika kuteua Mwanasheria Mkuu. Na siku iliyofuata (Ijumaa) akaonyesha yeye ni Rais wa aina gani kwa kufanya ziara ya ghafla kwenye Wizara ya Fedha na kujionea aina ya watendaji waliopo. Yote haya yanatosha