Amini usiamini mtu wangu, Rais wa Markani, Barack Obama ni miongoni wa viongozi wachache wa dunia wenye upendo mkubwa sana na muziki wa kizazi kipya na miondoko anayoikubali zaidi ni fleva za HipHop!
Nimekutana na stori ya Rais Obama inayoweka headlines za kila aina kwenye mitandao ya Marekani… je unajua ya kuwa Rais Obama anasikiliza sana muziki wa HipHop na kwa mwaka huu wa 2015 best ama favorite song wa Rais huyo wa Marekani ni..? Ipokee hii.
Nimekutana na interview aliyofanya Rais Barack Obama na jarida la PEOPLE Magazine, na humo Obama aliweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa sana wa rapper Kendrick Lamar na kwa mwaka huu wa 2015 wimbo wake wa ‘How Much a Dollar Cost’ ndio wimbo unaochezwa zaidi kwenye playlist yake.
Kwenye mazungumzo na jarida hilo Rais Obama alisisitiza kuwa wimbo huo umebeba ujumbe mzito sana na hajawahi kuchoka kuusikiliza na kila anapokuwa free basi hiyo ndio ngoma anayopenda kuisikiliza zaidi, huku mke wake Michelle Obama anaukubali sana wimbo wa Bruno Mars ‘Uptown Funk’ na kusema huo ndio wimbo wa mwaka kwa First Lady huyo.
Licha ya hayo kwenye playlist ya Rais Barack Obama majina ya mastaa hawa ni lazima ukutane nayo; Beyonce Knowles, Justin Tmberlake, Frank Ocean, Erykah Badu, Mary J Blige na Mos Def.
Usikilize wimbo huo wa Kendrick Lamar (How Much A Dollar Cost) hapa chini: