Kwakweli Kuitawala Tanzania ni Kazi Nyepesi Sana..Anachokifanya Magufuli Kwa Sasa ni Hichi - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Dec 2015

Kwakweli Kuitawala Tanzania ni Kazi Nyepesi Sana..Anachokifanya Magufuli Kwa Sasa ni Hichi

Wahenga walisema adui muombee njaa, lakini la pili na lipenda sana kuliko la kwanza " ukitaka kumtawala mwanadamu siku zote mnyime elimu bora"

Katika miaka hii ya 2015-2020 ndo miaka ambayo Tanzania ilipaswa kuionyesha dunia kwamba, inajitambua na inajielewa na imechoka kuendeshwa kwa matukio inataka mabadiliko ya kiuchumi na kimfumo. 

Hasa tujirejea 2005 na mwanzoni kwa miaka ya 2006 ambapo kwa kile kilichoitwa kasi ya viwango! kuna watu walikimbia mahoteli yao na mabiashara makubwa wakihofia kuingia mikononi mwa Serikali ya ari mpya nguvu mpya na kasi mpya! Vikao vilikua haviishi ngurudoto vamia vamia maofisini zilikua ni tabu, lakini saivi Raisi huyohuyo kuna watu wanaomba anyang'anywe hati yake ya kusafiria! Amazing!

Magufuli tangu ameanza kazi Ana mwezi na siku kadhaa sasa, na kazi yake tunaiona tumeona hata waziri mkuu akitembea na vinondo alivyopewa na wafanyakazi wema wa bandari na TRA na yeye kuvamia hayo maeneo na kuwachukulia hatua mara moja wahusika walioorodheshwa kwenye nondo zake! Well and good.. 

Ninachojiuliza ni Waziri gani wa nchi hii au naibu wake (waliopita) katika secta yoyote kati ya zilizoonyesha ubadhilifu mkubwa ambaye hata kuitwa kutolea ufafanuzi wa kinachoendea ameitwa? Lakini mtanzania huyuhuyu aliyeongozwa kwa style hizihizi zaidi ya miaka 54 sasa amevurugwa kabisa kana kwamba kinachofanyika sasa sio wajibu wa kiongozi na anapokea mshahara wake!

Nini madhara ya sifa hizi ambazo mimi nikiangalia huko dodoma watoto zaidi ya 50% wanazaliwa na mtindio wa ubongo sijaona mikakati ya kiubunifu ya kuliokoa taifa, Zanzbar saivi utadhani sio sehemu ya muungano na huyuhuyu mpewa sifa tangu akae Magogoni hakawahi hata kutoa kauli! Madhara ya sifa ni kwamba mwanadamu mwenye uwezo wa kucheza na akili za watu ambao wengi tumenyimwa elimu bora, ataona adhma yake imetimia na sasa ananafasi kwenye nafsi hizi zilizopoteza mwelekeo, ataendelea na style hiyohiyo huku akifukia mambo ya msingi yanayo muhusu mtu katika maisha ya kila siku! Na mara nyingi style za namna hii hufanywa na watu ambao wana "lack of creativity"

Huko mbeya kuna watu bado wanapenda kujifungulia Zambia kwasababu ya ubovu wa Hospitali za taifa so shame!

Kila kukicha thamani ya shilingi inazidi kuporomoka na bidhaa zinapanda bei Magufuli alivyoingia Ikulu sado ya viazi ilikua 3500 saivi 5000 sioni mkakati wa kuliokoa taifa na huu mfumko wa bei ukiuliza utaambiwa bado mapema tunasahau kwamba, wafanyabiashara ni wajanja bei ikishazoeleka wanaifanya ya kudumu,

Hadi saivi anachokifanya Magufuli, Majaliwa na Sef ni kuikosoa serikali iliyopita hakuna hata kimoja cha kwao walichokifanya taifa kuwa mahala salama pa kuishi,

Hapa juzi tu tuliambiwa serikali inatoa ada elekezi kwa shule binafsi hii inaleta picha gani? Hii ni tafsiri kwamba hakuna ubunifu wowote wala maono yoyote ya mzazi juu ya namna gani ya kuifanya elimu ya Tz kuwa bora hasa kupitia shule za umma! Japo tena hao hao wamekanusha kuingilia shule binafsi! "Contradiction"

Kuna watu nikiandika post zangu badala ya kufikiri kwa kina wanakimbilia kusema nimetumwa! Shauri yenu ujinga mwingine huo, na kwa taarifa yenu mi ni mtanzania huru kabisa ninaye waza tu hatima ya nchi yangu

Hii nchi inasafari ndefu sana kwa watu makini kuanza kumsifia mwanadamu yeyote! Tusichokijua tz ni kwamba, wanasiasa ni werevu sana hutafuta jambo ambalo anajua akilifanya watu wanaowaza kirahisi rahisi atakua ameteka akili zao na kufukia hata yale ambayo ni mahitaji yao ya msingi bila wao kujua "Dont play with Politicians they know how to play with your minds"