Nitahakikisha nakupatia kila stori inayonifikia….sasa hivi nakusogezea hii stori kutoka shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhusu kuwasimamisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.
Akizungumza leo Dec 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema…’Ukiacha kero zinazosababisha na Miundombinu TANESCO inachukua hatua madhubuti za kuwaadhibisha wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa wateja baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa pamoja na lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma kucheleweshewa huduma, ubadhirifu‘ – Mramba
‘Shirika linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa tayari limeanza kuchukua hatua kali kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na mambo hayo’ – Mramba
Kwa mfano katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na vyombo vya habari jana.Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, wahandisi na wahasibu’ – Mramba
‘Shirika litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi yeyote atakayebainika analaghai wateja, anadai rushwa anatoa lugha chafu au huduma mbovu atawajibishwa mara moja na pale atakapobainika kuachishwa kazi‘Mramba