Katika hali inayoashiria kuwa CCM haijajifunza somo kuwa wananchi wamekerwa na ufisadi.
CCM inataka kuwafanya wananchi wakose matumaini kwa serikali yao, na hivyo kupelekea kuona kuwa juhudi za Raisi Magufuli ni hatua za kuwabana dagaa huku wakiyaachia mapapa yakitanua mtaani.
Hatua hiyo ya kamati kuu ni hatua ya hatari sana kwa sababu inaweka maslahi ya watu wachache mbele kuliko Taifa, Hili ni jambo la kutisha na kuogofya sana, kama chama kilichojinadi kurudi katika misingi kinawalinda watu ambao Kwa kutumia nyadhifa zao wameifikisha nchi katika hali mbaya,basi ni jambo la kuwakatisha tamaa na kuwanyong'onyesha wananchi walioanza kurejesha imani kwa serikali yao.
DKT Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta ambao walikuwa mawaziri wandamizi kwenye Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao kwa sasa wanatuhumiwa kwenye Kashfa za ufisadi, imefichukua kuwa uwezekano wa kupandishwa mahakamani watu hao umeyeyuka. Mtandao umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Sababu iliyotajwa ya kuwaokoa mawaziri hao imetokana na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM,CC kilichoketi jana kimekuja na mipango mahususi ya kuwaokoa viongozi hao wanajiita na kuitwa ni waadilifu.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Kikao hicho ambazo zimevuja zinasema Kamati ya CC licha ya kujadili mambo mbali mbali ila jambo la ufisadi ambao uliibuliwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Kashfa ya ununuzi wa mabehewa 250 ya mizigo pamoja na Mabehewa 50 ya kubebea mafuta ambayo yamebainika kwa sasa ni mabovu nalo lilizungumziwa.
Chanzo chetu hicho kilichokuwa ndani ya CC kimedai kuwa viongozi wa mkutano huo walitaka suala la kuwachukulia hatua mawaziri hao waliokushika nafasi ya wizara ya uchukuzi,litazamwe kwa umakini kwani linaweza kukiingiza chama hicho tena kwenye mgogoro.
Yaani CC wameona hawa wakina mwakyembe na Sitta wakipandisha Mahakamani kujibu tuhuma hizo,basi chama chetu kitaingia kwenye mgogoro ambao unaweza hata ukapelekea idara hata ya Ikulu ya kipindi kile kufika mahakamani maana ufisadi huu wa Mabehewa ni mkubwa sana na umefanywa na mtandao mkubwa ndani ya nchi kimesema Chanzo chetu hicho.
Hata hivyo Kamati hiyo ya CC licha ya kuwakingia kifua mawaziri hao kunakuja ni ikiwa ni siku moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvunja Bodi ya Bandari ambayo Samwel Sitta wakati yupo Uchukuzi aliiunda Bodi ambayo Magufuli ameivunja kutokana na kuhusika kwenye ufisadi,
Hatua nyingine kwa bandari hiyo ni Rais Magufuli kutengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Bandari Awadh Massawe baada ya kubainika pia ameshindwa kuisimamia Bandari hiyo kwa kupelekea Ufisadi wa kutisha ikiwemo upotevu wa Kontena zaidi ya 2000.
Sanjaria Bandarini hapo Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi,Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi Shaaban Mwinjaka kutokana na kuitia hasara serikali ya bilioni 16 kwenye sherika la Reli ya Kati TRL.
Taarifa zilizopatikana wiki iliyopita zilisema Rais Magufuli alikuwa tayari amekabidhiwa ripoti ya Ufisadi wa Bandarini na TRL ambao unatajwa kuwa kwa namna yoyote uwezi ukawaacha mawaziri wenye dhamana ya Uchukuzi,
Hata ufanyaje ndugu,kwenye ufisadi wa huu wa kutisha lazima Sitta na Mwakyembe watawabwa Msalabani tu, maana wakati makontena hayo yanapoteka kati ya 2014 na 2015 mawaziri hawa walikuwepo uchukuzi hivi hawakuyaona haya au nao kuhusika katika kubariki wizi huu,harafu ukitoka kwenye Bandari unakuja kwenye TRL hapa ndio kuna madudu ambayo yanawaacha watupu,wanaojiita wapiganaji wa ufisadi amesema Mchambuzi wa Siasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma ,John Shilima.