Wema Sepetu Akiwa na Mtoto |
Kwa mujibu wa shosti wake wa karibu, kwa sasa Wema ameongeza urafiki kwa akina mama wenye watoto wachanga ili kuchukua ‘maujuzi’ ya namna ya kuwa mama bora kwa mwanaye mtarajiwa.
“Yaani ukitaka kujua Madam yupo bize na mazoezi ya kulea, kila tunapokwenda akimuona mama aliyemzoea mwenye mtoto basi ataomba ambebe mtoto acheze naye au hata amlishe.
“Kweli Wema anapenda watoto lakini sasa hivi imekuwa too much (imepitiliza). Hata ukifuatilia kwenye akaunti zake kwenye mitandao ya kijamii utaona sasa hivi yupo bize kutupia picha akiwa amebeba watoto,” alisema shosti huyo wa karibu wa Wema na kuongeza:
“Kiukweli bidada (Wema) yupo kwenye mazoezi makali ili awe mama bora kwa mwanaye mtarajiwa kwani alitamani kuwa na mtoto kwa muda mrefu.”
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti lilimtafuta Wema ili kujua anaendeleaje na mazoezi ya kulea mwanaye mtarajiwa lakini simu yake iliita bila kupokelewa.