Mwaka jana (2015) tulishuhudia producer na rapper Swizz Beatz wa Marekani ambaye ni mume wa muimbaji wa RnB, Alicia Keyz walidhihirisha hadharani kuwa wao ni mashabiki wa kazi za Diamond Platnumz kwa kupost video wakiwa wanasikiliza nyimbo zake (Ingia hapa).
Hiyo ilikuwa ni dalili kwamba kuna siku Swizz Beatz na Diamond wanaweza kuja kufanya kazi endapo itatokea wamekutana. Lakini kabla hata hawajakutana tayari mtayarishaji huyo ameonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Simba.
Diamond amesema kuwa Swizz alimtafuta hivi karibuni na kumwambia inabidi wafanye kazi,
Katika maelezo yake Diamond pia ameweka wazi kuwa anampango wa kwenda Marekani kushoot video ya collabo yake na Ne-Yo mwezi wa tatu, na alimwambia Swizz kuwa atakapokwenda kwaajili ya video hiyo ndio anafikiria wafanye kazi pia.
Katika collabo hiyo Platnumz amesema pia ana mpango wa kumuomba Alicia Keyz aimbe kiitikio kwenye collabo hiyo na Swizz.
Katika hatua nyingine, Diamond amesema kuwa ana collabo nyingine na msanii wa Marekani ambaye hata hivyo hakupenda kumtaja kwa sasa.

“Kuna Collabo na watu wengi sana Kwa mfano kama juzi kati nafikiri, kama siku tatu nyuma hivi Swizz alinicheki akaniambia itabidi tufanye kazi, nikamwambia sawa, na tuko tunaplan,” alisema Diamond kupitia Ayo TV.
Katika maelezo yake Diamond pia ameweka wazi kuwa anampango wa kwenda Marekani kushoot video ya collabo yake na Ne-Yo mwezi wa tatu, na alimwambia Swizz kuwa atakapokwenda kwaajili ya video hiyo ndio anafikiria wafanye kazi pia.
“Nikamwambia mimi nakuja Marekani nafikiri mwezi wa tatu kama sijakosea, au before mwezi wa tatu, kwasababu kushoot video yangu niliyofanya na Neyo, ndio tunaenda kushoot video, nikamwambia nikija ndio itakuwa time nzuri tunafanya hapo hapo”.