Msanii wa Muziki Niki wa Pili Aikosoa Serikali Kuhusu Kuzuia Bunge Kurushwa Laivu - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Jan 2016

Msanii wa Muziki Niki wa Pili Aikosoa Serikali Kuhusu Kuzuia Bunge Kurushwa Laivu

Msanii wa muziki wa bongo kutoka katika kundi la Weusi, Niki wa pili amefunguka na kusema kuwa serikali kabla ya kufanya maamuzi ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge kurushwa kupitia Televisheni ya taifa walipaswa kwanza kuwauliza wananchi.

Niki wa Pili amesema hayo kupitia Account yake ta Twitter baada ya serikali kuweka msimamo wake kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kupunguza gharama za urushaji wa matangazo hayo.
Niki wa pili ameeleza kuwa sababu nyingine iliyotolewa na serikali kuwa watu wengi huwa hawapati muda wa kuangalia shughuli za bunge si za kweli kwani watu huwa wanapata muda wa kufuatilia bunge hilo.

“Sisi walipa kodi ndio tungeulizwa kwanza, je kwa hizi gharama tuoneshwe bunge au hapana…mbona makampeni pia yalikuwa gharama kubwa, Bunge huwa linaangaliwa sana, sehemu nyingi unakuta wame tune…so wangetafuta matangazo ya biashara ku cover gharama hizo” Alisema Niki wa Pili.

Jana serikali kupitia kwa waziri Nape Nnauye ilitoa taarifa ya kuzuia bunge kurushwa live kupitia Televisheni ya taifa na badala yake walisema bunge litakuwa linarekodiwa na kurushwa kwenye kipindi maalum kupitia televisheni hiyo ya taifa kuanzia saa nne usiku mpaka saa tano za usiku, na kusema kuwa kipindi cha maswali na majibu tu ndio kitakuwa kinarushwa live jambo ambalo limepokea tofauti na watu huku wengi wao wakionesha kutofurahishwa na maamuzi hayo ya serikali.