DIAMOND Platnumz Ashutumiwa Kuwabania Wenzake Connection za nje...Mwenyewe Adai Anatumiwa na MTV Base Kupitisha Video za Kuchezwa Kwenye TV Hiyo - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Jan 2016

DIAMOND Platnumz Ashutumiwa Kuwabania Wenzake Connection za nje...Mwenyewe Adai Anatumiwa na MTV Base Kupitisha Video za Kuchezwa Kwenye TV Hiyo


Kama Diamond akisema ‘Hapana’ huenda video ya msanii wa Bongo isipate mwanga wa siku kwenye playlist za kituo cha runinga cha MTV Base.

Hata hivyo amesema nafasi hiyo huitumia kuwabeba wasanii wengi wa Bongo Flava kwa kadri awezavyo.

Alisema anawashangaa wasanii wanaomtupia maneno kila kukicha kuwa anawabania wasanii wengine ‘connections’ za kung’ara kimataifa.
“Mimi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mi najitahidi kuwasaidia wenzangu tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mi ndio huwa nasababisha,”alisema.

Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwa sababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yeyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? Tuicheze ngoma yake au? Mimi huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu?”

Pia Diamond alisema timu yake ya Wasafi ndiyo ilivishauri vituo vya runinga vya Sound City na MTV kuanzisha chati za Afrika Mashariki.