Kulihitajika Uchunguzi wa Kina Dhidi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Dr. Faisal Kwanza Kabla ya Kufukuzwa - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Jan 2016

Kulihitajika Uchunguzi wa Kina Dhidi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Dr. Faisal Kwanza Kabla ya Kufukuzwa

Ukweli ni kuwa kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Dr. Faisal kumeambatana na ukiukwaji mkubwa wa maadali ya utumishi wa umma! Dr. Faisal amefukuzwa kazi kwa kuegemea ushahidi wa upande mmoja huku chanzo cha kufukuzwa kwake kikiwa hakijawekwa bayana! Hili ni tatizo kubwa! 
Tunaambiwa kuwa rais Magufuli alichukuwa uamuzi wa kumfukuza kazi mtumishi huyo wa umma muda mfupi sana baada ya kupokea simu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza ndugu Magesa Mlongo! 
Kimsingi rais alitakiwa kupima kwa kina aina ya mtu anayempa maelezo! Magesa Mlongo !mashitaka yake kwa rais yalitakiwa kupimwa kwa umakini mkubwa! Kulitkiwa subira na uchunguzi wa kina hasa ikizingatiwa historia aliyo nayo ndugu Mlongo!
Tungependa kuona haki inatendeka na utu unalindwa dhidi ya hili!
By G Sam From Jamii Forums