Mama Kaniletea Mke Kutoka Kijijini Bila Ridhaa Yangu, Nifanyeje? - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Jan 2016

Mama Kaniletea Mke Kutoka Kijijini Bila Ridhaa Yangu, Nifanyeje?

Wadau mwishoni mwa December mama alikuja hapa dar na mgeni, walifikia kwangu, mgeni mwenyewe ni binti wa kama miaka 20 hivi, nilishangaa maana mama akija Dar hufikia kwa mkubwa wangu, kaka, mimi huenda kumuona huko
Cha kushangaza safari hii, mama akafikia kwangu pamoja na huyo mgeni wake, nilipomuuliza kuhusu huyo binti mama akadai wana mambo yao yaliyowaleta, after some days mama akaaga anaenda kuwasalimia familia ya kaka yangu atakaa siku kadhaa, ila atamuacha binti hapa kwangu kwa siku tatu nne
Nilipoachwa nae binti, roho ya shetani ikatamalaki, nikamrubuni yule binti hatimaye tukashiriki ile dhambi pamoja bila kujua ni mtego eti kumbe mama kamuacha kama mke wangu, nikamuhamishia chumbani kwangu ili nimfaidi sana pindi mama akija kumchukua niwe mwepesi
Kuja kustuka ni wiki mbili zimeisha tangu binti kuhamia room kwangu na tangu mama aende kwa kaka kimara, mm naishi kigamboni, kukawa na kila dalili Girlfriend wangu atakuja siku moja kumkuta binti hapa halaf iwe shida, nikaona nipige simu kwa kaka kuuliza mama anakuja kumchukua huyu binti lini, kaka alishangaa mno, akasema mbona mama alishaondoka wiki nzima nyuma kurudi village na kwamba huyo binti ni mke wako amekuletea na wewe umekubali na amewaacha kwa furaha, nikachanganyikiwa
Kumbe ndio maana simu ya mama haikupatikana kwa wiki mbili
Wadau nimechanganyikiwa, sasa jana nimempata mama hewani ananiambia huyu ndio mke wangu, ana tabia nzuri, kuwa ni mtoto wa flani wanamjua tangu kuzaliwa, kwamba hata baba karidhia na ndie aliewasafirisha, kwamba wamenivumilia muda mrefu nipo nipo tu hivyo waniletee mke
Naombeni msaada