Jeshi la Polisi Jumatatu hii limezima ghasia za wananchi wenye hasira maeneo ya Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam baada ya kupinga zoezi la bomoa bomoa kwa mara ya pili kufuatia kukataa kuondoka katika eneo hilo kwa madai hawana pa kwenda.
Bi Fatuma akizungumza kwa uchungu
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii mmoja kati ya waathirika wa bomoa bomoa hiyo, Bi Fatuma Said, amesema wanashindwa kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa hawana sehemu ya kwenda huku akiitaka serikali kuwafikiria.
“Sio kwamba tumegoma kuondoka wengine sisi hatuna sehemu ya kwenda,” alisema. “Sisi baada ya kubomolewa nyumba yetu tukashindwa kuondoka kwa kukosa pa kwenda.Tukaamua kujenga hapa vijibanda ili serikali itufikirie lakini tunashangaa leo asubuhi vibanda vyetu vimewekwa X kwamba wanataka kubomoa. Saa tano tumeingiliwa kwenye vibanda vyetu sisi tukakimbia wao wakachoma ndio baadhi ya wanacnhi wakaingiwa na hasira na kwenda kuchoma matairi barabarani,”alieleza.
Hata hivyo Bongo5 ilijaribu kuzungumza na afisa wa polisi aliyekuwepo katika eneo hilo, lakini alisema watatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo. Hadi sasa polisi wanawashikilia vijana kadhaa wanaohusishwa na tukio hilo.
Tazama picha zaidi: