Rais Magufuli Apewa Jipu Gumu Sana Alitumbue..Ni Jipu Linalosumbua Wananchi Wengi Sana - MULO ENTERTAINER

Latest

5 Jan 2016

Rais Magufuli Apewa Jipu Gumu Sana Alitumbue..Ni Jipu Linalosumbua Wananchi Wengi Sana

Mh. Rais naomba uliangalie kwa makini jipu kuu la utosi linalotutesa wananchi wako! Ada za shule, zahanati kila kijiji au ujenzi holela mabondeni hayo ni matokeo tu ya jipu kuu!Jipu hilo ni kiwango cha juu cha riba ya mikopo kwa watumishi wa umma na watanzania wengine wa kipato cha kati-chini na chini kabisa!

Banks zinakata hadi 20% na makampuni binafsi yanafikia hadi 40%, kwa jinsi hii hakuna jinsi kundi hili kubwa ktk jamii yetu litaweza kushiriki ktk kujenga uchumi!

Nakuapia kwa pesa za makontena na walipa kodi wengine wachache ndani ya nchi haziwezi kukufanya uboreshe huduma za jamii, ada itaichemsha serikali yako hata bila ya kuizungumzia afya!
Mfano bora, tazama elimu ya chuo kikuu, wengi wame afford thru mkopo! Hao hawaisumbui tena serikali kwa kuwa kama marejesho yatasimamiwa then watu watajisomesha! 

Ujenzi holela utakufa tu pale nitakapopata mkopo na kuweza kumudu gharama ya kiwanja kilichopimwa! Hata wakulima wetu wataboresha pembejeo!

Sio kama watanzania niliowasema hapo juu hawakopi, la hasha Hawa ndio wanaokuza sekta ya microfinance na bank nyingi nchini huku wakikuibia muda serikali kufanya vijikazi vya kimachinga kuikimbiza riba ya hayo mabank au makampuni binafsi!

Hazina ilitoa mikopo yenye riba ya 5% kwa baadhi ya watumishi wengi walikopa na sidhani kama serikali ilifilisika kwa hilo!

Hebu kakae na boss mpango muone ni jinsi gani mabank yetu yaweze kuleta tija kwa wananchi na yasiwe mwiba!

Kwa mnaoishi Europe na sehemu nyingine za dunia hebu semeni experiences zenu na mikopo na jinsi inavyowakomboa wananchi na serikali zao!

Mh. JIPU HILI LIKITUMBUKA nitakuwa nacheka ninapoenda TRA au mamlaka yeyote kulipa kodi!