ROSE NDAUKA Afunguka Kuhusu Nyumba yao Kubomolewa...Adai Hawezi Shikwa na Presha Kama Wastara - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Jan 2016

ROSE NDAUKA Afunguka Kuhusu Nyumba yao Kubomolewa...Adai Hawezi Shikwa na Presha Kama Wastara

WAKATI mamia ya wakazi wa Dar es Salaam waishio mabondeni na pembezoni mwa bahari na mito wakihaha nyumba zao kuvunjwa, staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hajali kama nyumba yao itakutwa na bomoabomoa hiyo.

Badala yake, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kusimamia zoezi hilo, kwani wengi wa wanaobomolewa walishapewa taarifa mapema na hawakutii agizo hilo la serikali, lakini akaitaka kuwaangalia kwa jicho la tatu watu ambao hawakupewa taarifa za zoezi hilo.

 “Wazazi wangu wakibomolewa nyumba naona kawaida tu, siwezi kuwa na presha maana kila kitu kinapangwa na Mungu, kama ni kubomoa wabomoe tu hatuna la kufanya,” alisema Rose.

Global Publishers