Serikali ya Eritrea yatoa Amri Kila Mwanaume Kuoa Wake Wawili - MULO ENTERTAINER

Latest

27 Jan 2016

Serikali ya Eritrea yatoa Amri Kila Mwanaume Kuoa Wake Wawili

Wanawake wa Kieritrea
Huko nchini Eritrea, serikali imetoa tangazo kuwa, LAZIMA KILA MWANAUME, AOE MKE WA PILI. Hali hii imejitokeza baada ya kuwa na upungufu wa wanaume, kulikosababishwa na wengi kufia vitani wakati wa vita kati ya nchi hiyo na Ethiopia!

Serikali imetoa tangazo kwa Lugha ya Kiarabu, na kwa mujibu wa Tangazo hilo mwanaume atakayepuuzia agizo hilo, "atahukumiwa kwenda jela, pamoja na kazi ngumu".

Na mwanamke atakaye fanya juhudi zozote kumzuia mwanaume wake asioe bibi wa pili, adhabu yake ni "kifungo cha maisha gerezani", ili akose mume kabisa, ajue uchungu wa mwanamke mwenzie kuishi bila mwanaume.

Habari hii imekuwa , habari njema nchini Kenya, baada ya Wakenya kuanza kuomba Visa za kuingia nchini Eritrea na kuanza taratibu za kubadili urai, ili waweze kuoa wake wawili, baada ya kule Rombo watu kuanza kuchangamkia wake zao vilivyo, fursa zimehamia Eritrea.

Je, hapa Tanzania kuna haja, ya serikali pia kutangaza au kutoa agizo kama hilo..? Uhaba wa wanaume upo, japo chanzo kikuu hapa kwetu ni upungufu wa nguvu za kiume, pamoja na uoga wa maisha plus majukumu.