Jana usiku klabu ya Real Madrid imefanikiwa kutetea kombe la klabu Bingwa barani Ulaya kwa kuitwanga Liverpool goli 3-1 . Real Madrid ambao dakika 20 za kwanza za mchezo huo walionekana kuelemewa na Liverpool lakini hadi mapumziko hakuna klabu iliyokuwa imeona lango la mwenzake.
Kipindi cha pili Real Madrid walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Benzema, goli ambalo lilikuwa ni uzembe wa goli kipa wa Liverpool, Loris Karius ambapo alirusha mpira karibu na miguu ya Benzema kunako dakika ya 51.
Goli hilo halikudumu sana kwani dakika 4 mbele mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane akaisawazishia timu yake.
Mchezo ulianza kubadilika na kuwa mgumu kwa Liverpool baada ya mshambuliaji wake tegemezi, Mohamed Salah kuumia beka na kutoka Uwanjani.
Real Madrid wakaonekana kubadilika na pengo hilo liliwasaidia kupata magoli mawili ya haraka kupitia kwa Gareth Bale.
Kwa mujibu wa mtandao wa Liverpool Echo Mohamed Salah ana asilimia 51 za kwenda Urusi kushiriki kombe la dunia hii ni kutokana na majeraha aliyoyapata jana.