Kupitia ukurasa wake wa Facebook muda mchache uliopita, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameweka picha yake na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kuandika hivi; "Mimi binafsi siwezi kuwa mfungwa wa magomvi yetu ya miaka ya nyuma. Nilishasamehe walionikosea…Mbowe siku zote amekuwa Kiongozi wangu na siwezi kubeza nafasi yake katika kujenga demokrasia nchini. Tulipishana. Tulikoseana. Tusameheane"
Tulia utafakari, halafu tupe maoni yako
Tulia utafakari, halafu tupe maoni yako