Edward Lowassa: Tutaingia IKULU Kwa Amani Bila Kumwaga Damu - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Feb 2016

Edward Lowassa: Tutaingia IKULU Kwa Amani Bila Kumwaga Damu

Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa chama hicho, jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana walipomtembelea ofisini kwake amewataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.

Lowassa pia ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.

Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watazania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."