Kauli ya Rais Imevunja Katiba; kwa Kuingilia Uhuru wa Mahakama - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Feb 2016

Kauli ya Rais Imevunja Katiba; kwa Kuingilia Uhuru wa Mahakama

Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mia mbili.

Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;

1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.

2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.

3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.

4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.

5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??

Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;

Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.

(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;

Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.

Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.

Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.

Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.

Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.

Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.