Jay Z amshtaki mwanamuziki Rita Ora - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Feb 2016

Jay Z amshtaki mwanamuziki Rita Ora

Mwanamuziki Rita Ora
Kampuni ya kurekodi ya Jay Z's Roc Nation, imemshtaki mwanamuziki Rita Ora ikidai alivunja kandarasi yake mbali na kutotengeza idadi ya albamu alizoahidi.
Kesi hiyo imeanzishwa mjini New York wiki sita baada ya Rita kuanzisha mashtaka dhidi ya kampuni hiyo mjini Los Angeles.
Rita anadai kwamba kampuni hiyo ina kandarasi haramu naye na kwamba anaomba kutoka.
Rita Ora alijiunga na kampuni hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na alikuwa miongoni mwa wanamuziki wa kwanza kusajiliwa na Jay Z.
Tangu ajiunge na kampuni hiyo ya kurekodi muziki ,Rita ametoa albamu moja ya kibinafsi ambayo ni yake ya kwanza mwaka 2012.
Image copyrightReuters
Image captionRita Ora
Hatahivyo kampuni ya Roc Nation imesema itataka kulipwa dola milioni 2.4 ikisema kuwa imetumia zaidi ya dola milioni 2 kutengeneza na kuiuza albamu ya pili ya mwanamuziki huyo ambayo haijatoka.
Kulingana na ukurasa wa sita wa gazeti la The New York Post,kampuni hiyo inadai kwamba mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 aliingia katika kandarasi ya kutoa albamu tano na kampuni hiyo lakini ametoa albamu moja kufikia sasa.
Roc Nation inasema kuwa ilimsajili Rita Ora alipokuwa hajulikani na imemuuzia kazi yake na kuwekeza mamilioni ya madola za kurekodi na gharama nyengine hivyobasi kumsaidia Bi. Ora kupata ufanisi na kuwa maarufu .
Wakili wa mwanamuziki huyo ,Howard King,alisema:Jay Z binafsi amemuahidi Rita kwamba atamwachilia huru kutoka katika Roc Nation,maelezo ambayo yanaendelea kufanikishwa.
Image copyrightAP
Image captionJay Z na mkewe Beyonce
Tunaamini kwamba wasambazaji wa muziki wa Roc Nation,Sony Music imeaigiza Roc Nation kuanzisha mashtaka haya ili kulinda haki za Sony.
Muziki wa Rita Ora bado unaendelea kusambazwa na kampuni ya Sony,licha ya kubadilisha wasambazaji hadi kwa kampuni ya Universal mwaka 2013.