Mkongwe kwenye sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amevunja ukimya na kuweka bayana kuwa miaka kadhaa iliyopita aliwahi kumchuna sana Mkurugenzi wa Kampuni ya Watanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma alipokuwa akimhitaji awe mchumba wake.
Johari alifunguka hayo hivi karibuni baada ya mwanahabari wetu kumfungia safari hadi ofisini kwake Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam na kumuuliza juu ya taarifa zilizokuwa kwenye makabrasha yetu kwamba mwigizaji huyo miaka kadhaa iliyopita, aliwahi kumchuna sana Ostaz Juma lakini habari hizo hazikuandikwa gazetini.
Johari alifunguka hayo hivi karibuni baada ya mwanahabari wetu kumfungia safari hadi ofisini kwake Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam na kumuuliza juu ya taarifa zilizokuwa kwenye makabrasha yetu kwamba mwigizaji huyo miaka kadhaa iliyopita, aliwahi kumchuna sana Ostaz Juma lakini habari hizo hazikuandikwa gazetini.
“Mh! Jamani hayo mambo ya zamani. Ujue watu wamekuwa wakinisumbua sana na ishu ya kusema mimi niliwahi kutoka kimapenzi na Ostaz Juma Namusoma jambo ambalo si kweli, Ostaz Juma aliwahi kunitongoza siku nyingi sana bado nipo Kaole na alikuwa akija mazoezini karibia kila siku ila mimi nilikuwa simtaki hata kumsikia.
“Kutokana na kuwa na mkatalia mara kibao kwa kuwa alikuwa na fedha alikuwa akinipatia fedha si unajua yule ni tajiri, ukipiga hesabu vizuri kama ningekuwa najenga basi leo hii ningekuwa hata na maghorofa mawili kupitia fedha alizokuwa akinipa, alikuwa ananipatia kila siku ya Mungu fedha na marafiki zangu pia ila mimi tu nilikuwa nikimkataa hivyo kuwafanya marafiki zangu kunishangaa ingawa na wao walinufaika.
“Ostaz Juma alikuwa na kawaida ya kunifuata kila siku mazoezi huko Kigogo na akija ananinunulia kila kitu na mara nyingine ananikodia usafiri wa kunirudisha nyumbani lakini pamoja na hivyo niliishia kutumbua fedha zake nyingi na hakuweza kunipata jambo ambalo aliendelea kunisisitizia kuwa lazima siku moja angeweza kuwa na mimi japo hakufanikisha kunipata,” alisema Johari. Ostaz Juma ambaye amekuwa akiwasaidia wanamuziki mbalimbali nchini kifedha, hakutaka kuzungumzia ishu hiyo kwa kudai ni ya zamani sana, kwa sasa ameoa na anaendesha familia yake.