Picha ya Ziara ya Kwanza |
kakuta matatizo tele hasa amewakuta wamama waki share vitanda hadi watu watano
na wengine wakilala chini.....
Utakumbuka few months ago tulitangaziwa kuwa baada ya Magufuli kwenda Muhimbili
vitanda vilipelekwa hadi vikakosa wagonjwa
kuna picha zilisambazwa paka kalalia kitanda kipya Muhimbili
na kwamba sasa mambo ni tofauti kabisa...vitanda tele na kila kitu saafi
Sasa binafsi siamini kabisa Muhimbili imewahi kuwa safi na matatizo yakaisha
ambacho najiuliza why 'maigizo yale ya kuwa mambo ni saafi' yaliruhusiwa
kuendelea ?
why sisi wananchi na waandishi wa habari hatukupinga kabisa habari za kuwa
mambo ni saafi muhimbili?
why habari ya leo iwe kama habari mpya
while in reality watu wameendelea kulala chini tu kama zamani?
Inawezekana kabisa tatizo haliko kwa wanasiasa?
tatizo liko kwetu wananchi na hasa media?
tumeletewa 'sanaa tukaishangilia huku ukweli tunaujua'?
sababu muhimbili hali yake sio siri
lakini tulipoambiwa mambo sasa ni saafi tuliruka ruka na kushangilia...
huku kiukweli hali ni ile ile tu.....
Na leo tena wananchi wamemlilia tena Magufuli bila kujiuliza
ni kweli Magufuli hali iliyopo haijui?si alikwenda juzi tu hapo hapo Muhimbili?
au haya matatizo ni mapya kabisa?