Rais wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein atembelea Maskani ya Kisonge iliyopigwa bomu jana usiku...! - MULO ENTERTAINER

Latest

5 Mar 2016

Rais wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein atembelea Maskani ya Kisonge iliyopigwa bomu jana usiku...!

Kontena la Maskani ya kisonge Mjini Unguja liliolipuliwa kwa bomu na watu wasiojulikanwa usiku wa jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  pia  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)  akiangalia  hasara iliyopatikana katika Maskani ya Kisonge  iliyotokea jana kwa  mlipuko wa bomu uliosababishwa na watu wasiojuilikanwa, (wa pili kushoto) John Mwakanjuki akitoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  pia  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Maskani ya Kisonge John Mwakanjuki leo wakati alipotembelea maskani hiyo baada ya kutokea mlipuko wa bomu lilotegwa  katika ofisi hiyo na watu wasiojuilikanwa usiku wa jana.