Serikali Kutoa Mil.50 kwa Kata Zote Maskini Nchini - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Mar 2016

Serikali Kutoa Mil.50 kwa Kata Zote Maskini Nchini

Mkurugenzi Dawati la Wazee Tume ya Utumishi na Utawala Bora nchini Tanzania Bw. Joshua Tarimo amesema Serikali imeahidi kutoa shilingi milion 50 kwa Kata zote nchini lengo likiwa ni kupunguza umaskini hasa kwa wazee wasiojiweza kujikimu katika kupata mahitaji yao ya kila siku.
Bw.a Tarimo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wazee kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo lakuwasikiliza mikakati yao na mipango ambayo wanataka itekelezwe na kusimamiwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli.

Serikali imeahidi kutoa shilingi Milion 50 kwa Kata zote nchini lengo likiwa ni kupunguza umaskini hasa kwa wazee.
Mkurugenzi Dawati la Wazee Tume ya Utumishi na Utawala Bora nchini Tanzania Bw. Joshua Tarimo amesema Serikali imeahidi kutoa shilingi milion 50 kwa Kata zote nchini lengo likiwa ni kupunguza umaskini hasa kwa wazee wasiojiweza kujikimu katika kupata mahitaji yao ya kila siku.
Bw.a Tarimo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wazee kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo lakuwasikiliza mikakati yao na mipango ambayo wanataka itekelezwe na kusimamiwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Shirika la Saidia Wazee Tanzania SAWATA Bi. Clotilda Kokupima amesema bado wazee nchini wanakabiliwa na wanachangamoto kubwa sana ya kukosa haki zao kwa kutokuwepo kwa Sheria na Sera maalum ambazo zitalinda na kusimamia haki za wazee nchini na pia kuitaka Serikali itoe elimu ya ziada kwa jamii kuhusu imani potofu walizonazo juu ya wazee nchini.

Bi. Kokupima amesema katika tafiti walizofanya wamegundua kila siku Tanzania wanakufa wazee 283 kwa sababu ya kukosa huduma muhimu za kibinadamu hivyo Serikali inapaswa kuanza kuwatambua wazee nchini na kuwahudumia.