Serikali ya Tanzania Kuingiza Nchini Ndege 2 za Kisasa Kutoka Canada Ndani ya Siku 60 - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Mar 2016

Serikali ya Tanzania Kuingiza Nchini Ndege 2 za Kisasa Kutoka Canada Ndani ya Siku 60

Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano wa anga na Serikali ya Quwait.

Makubaliano hayo yatawezesha mashirika ya ndege ya nchi zote mbili kufanya safari za moja kwa moja na kukuza sekta ya utalii.

Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi imethibitisha kwamba imeagiza ndege za kisasa kutoka nchini Canada ambazo zinatarajiwa kuwasili nchini ndani ya siku 60 (miezi miwili ijayo).

Kwa kuanzia, awamu ya kwanza ya ndege hizo zitafanya safari za ndani bara na visiwani kabla ya kujitanua ndani na nje ya Afrika.

Shime watanzania, tusimame kidete na serikali yetu kuhakikisha kwamba tunaachana na unyonge wa kutumia ndege za mashirika ya nchi jirani. Hii ni fursa nzuri ya uwekezaji katika sekta ya chakula, nishati, vinywaji n.k.