Waziri Muhongo Amjia Juu Zitto Kabwe, ni Kuhusu Kampuni ya IPTL - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Mar 2016

Waziri Muhongo Amjia Juu Zitto Kabwe, ni Kuhusu Kampuni ya IPTL

SIKU chache kupita baada ya Mbunge wa Kigoma mjini,Zitto Kabwe kusema tangu utawala wa Rais John Magufuli kuingia madarakani,Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeitia hasara serikali ya Bilioni 36 kwa kile anachodai Kampuni hiyo inaitapeli serikali kwenye Malipo ya Capacty Charge,

Naye Waziri wa Nisharti na Madini,Sospeter Muhongo ameibuka na kusema Mbunge huyo anatumiwa kuisakama kampuni ya IPTL kwa maslahi yake kisiasa,

Waziri Muhongo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa Fullhabari.blogs mara baaada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari aliokuwa anazungumzia ugunduzi mpya wa Gesi asilia,

Ambapo Waziri Muhongo ni kama amemshangaa mbunge huyo kwa kitendo chake achodai ni kushikilia hoja ya IPTL kila siku badala ya kutamaza mikataba yote ya Makampuni ya umeme ambayo inauzia umeme Tanesco ambayo amekili ni mibovu,

“Yaani huyu mtu anaugomvi tu na hii kampuni na anaitumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa,maana kila siku yeye na IPTL tu,kama hoja ni mikataba ni mbovu,ni makampuni yote yanayoiuzia shirika la umeme Tanesco mikataba mingi inakasoro nyingi,lakini nashangaa huyu Zitto ayasema haya kila siku na IPTL,mbona mengine hasemi”amesema Waziri Muhongo,

Waziri Muhongo ameongeza kuwa “na nyinyi wanahabri tumieni elimu yenu kuelimisha umma,tuache kuingia kwenye mitego ya wanasiasa wa aina hii,tusema ukweli juu ya mkataba wa IPTL na Tanesco”

Kauli ya Waziri Muhongo inakuja ikiwa Mbunge huyo ambaye ni Kiongozi wa mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo kuandika kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36 kupotea,

"Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Raisq, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.

Aidha,Zitto Kabwe aliongeza kusema kuwa Wakati Rais Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini,

"Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi.

"Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini.