Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz amefunguka na kueleza jinsi wadau wa muziki nchini wanavyosababisha wasanii wa muziki kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya.
Rapper huyo ambaye ameachana na matumizi ya Madawa ya kulevya hivi karibuni, ameiambia BBC kuwa wasanii wengi wanaingia kwenye Madawa ya kulevya baada ya kupata stress za kubaniwa kwenye muziki.
“Watu wanamsongo wa mawazo, mashabiki wetu hawajui sisi jinsi tunavyodeal na watu ambao wanatufikisha kwao, wadau wa muziki, wadau wa muziki ni watu tofauti sana na wanafanya vitu vibaya sana,” alisema Chidi. “Wachache wapo wanaosaidia vizuri, lakini ni wengi wanaoharibu na wanaharibu sana sana, yaani mtu anakuwa na kisasi na wewe na yupo tayari kukufanyia kitu chochote, akushushe, akupinguze mpaka umalize pesa zote na usipingwe hata wimbo wako mmoja,”
Pia rapper huyo alisema wasanii wengi wanabaniwa kutokana na migongano ya kimaslahi katika kazi au kushare mademu na wadau wa muziki.
“Huu muziki tunaoufanya na haya maneno tunayoyaimba, kuna wale ambao wanachukulia starehe na kuna wengine wanachukulia unawasema au mabinti zao wanatupenda sisi wasanii. Unakuta kuna binti amekupenda wewe msanii, kumbe yule ana mtu mwingine au mdau, sasa huyo mtu akisikia kwamba Chidi Benz anadeal na mtu wake, hawezi kuelewa kwamba mtu wake ndio anamfuata Chidi Benz, ila yeye atakufanya kitu chochote kile ili akuumize au akuharibu na ‘akustopishe’ maendeleo yako. Na inawezekana yule mtu wewe haukudeal naye ila anakupenda tu kishabiki na anawaambia marafiki zake hivyo lakini marafiki zake inatokea wakaibadilisha na wakaiweka kimapenzi, tayari una vita na mtu wake ambaye anamwangalia,” alisema Chidi.
Pia rapper huyo amedai kilichomwingiza yeye kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya ni kutochezwa kwa ngoma zake kwenye redio na runinga hali ambayo ilimfanya ajione mpweke.