Picha:Uwoya Amtia Majaribuni Richie - MULO ENTERTAINER

Latest

27 Jun 2016

Picha:Uwoya Amtia Majaribuni Richie


Irene Uwoya na Richie.
WAKATI Waislam wakiwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya juzikati alimtia majaribuni msanii mwenzake Single Mtambalike ‘Richie’ walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar kulikokuwa na harusi ya mdogo wake Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Happy Mengere.

Kwenye ‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa amevalia kivazi kilichoacha mapaja yake wazi, alionekana mara kadhaa akimkumbatia Richie na hata paparazi wetu alipotaka kuwafutoa picha, staa huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu wakinong’ona chinichini.

“Uwoya hivi haoni anamtia mwenzake majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu analazimisha kupiga naye picha ya kumkumbatia, ila hawa wasanii wamezoeana sana,” alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa.

Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipojaribu kuwakaribia na kumuuliza Uwoya kulikoni anamfanyia mwenzake vituko alisema, alijisahau kuwa Richie yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila alipiga picha hiyo kama pozi la kawaida tu na wala hakuwa na nia mbaya.