Umaarufu wa Supu ya Pweza Kwa Wapwani..Je ni Kweli Inaongeza Nguvu za Kiume? - MULO ENTERTAINER

Latest

26 Jun 2016

Umaarufu wa Supu ya Pweza Kwa Wapwani..Je ni Kweli Inaongeza Nguvu za Kiume?



Ukitembea katika mitaa ya Mombasa na Pwani kwa jumla, utaskia wakaazi wakisema wametoka kunywa supu ya pweza.

Licha ya kwamba wengi wanamfahamu mnyama huyo wa majini kama kitoweo, umuhimu wa mnyama huyo kwa wapwani ni mkubwa mno baada ya wao kugundua kuwa ana faida zaidi katika maisha ya kila siku.

Wataalam wa sayansi wamedhibitisha kwamba nyama ya pweza pamoja na supu yake inaongeza madimi muhimu kwa binadamu, na la kuvutia zaidi ni kwamba husaidia kuimarisha nguvu za kiume.

Wanaume haswa hupenda kuitumia huku wakiamini kwamba inawasaidia kuwapa nguvu wakati wa kufanya mapenzi na wake wao.

Nilikutana na baadhi ya wavuvi mjini Mombasa na kutaka kujua ni kitu gani kinafanya supu ya pweza kuwa maarufu sana kwa wakaazi wa eneo hilo.

“Hapa Mombasa ukisema umetoka kunywa supu ya pweza utashangaa watu wakikuangalia mara mbili. Uwa tunaamini kwamba inaongeza nguvu za kiume na hii ndio sababu huwa tunapenda kuitumia,” alisema Omari, mmoja wa wavuvi hao.

Wakaazi hao walisema kuwa tofauti na watu wengine wanaotumia madawa ya kisasa ya kuongeza nguvu wakati wa tendo la ndoa, wao hutumia supu hiyo kujiimarisha wakati wa 'Dimba Uwanjani'.

“Mimi huwa nashangaa eti watu wanatumia sijui madawa ya kizungu ambayo baadae yanasababisha madhara ya kiafya. Waambie watu waje Mombasa hapa supu ya pweza ndio habari ya mjini,” alisema mvuvi mwingine.

Inaaminika kuwa baadhi ya wanawake hutengezea waume wao supu hiyo kila siku na kuwaandalia kila wanapotoka kazini ili kuhakikisha wanapata mchezo wa uhakika katika sita kwa sita....