Baada ya TID Kumwita Bill Nas Chawa...Bill Nas Afunguka na Kusema Haya Kuhusu TID - MULO ENTERTAINER

Latest

1 Jul 2016

Baada ya TID Kumwita Bill Nas Chawa...Bill Nas Afunguka na Kusema Haya Kuhusu TID



Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Bill Nas amesema TID ni mtu muhimu sana kwake kwani ana mchango mkubwa kwenye maisha yake na muziki wake kiujumla.

"TID ni mtu ambaye mi namuheshimu sana, ana mchango kwenye muziki wangu na mambo mengine, hata leo unaposikiliza ligi ndogo ni kati ya chorus kali sana ambazo mi naziheshimu sana, lakini kuhusu kutoka radar na vitu vingine, nilikuwa nataka nikutane naye mwenyewe kama mwanafamilia, kwa sababu naona ishu inaenda kwenye media", alisema Bill Nas.

Pia Bill Nas amesema hali hiyo inamuumiza hata kikazi pia, lakini ilimpasa kuondoka Radar, kwani muda wake wa kuwepo hapo ulishaisha.

"Kwa namna moja au nyingine hata mimi inanifrustrate sana kwa sababu kuna vitu vingi nataka kuvifanya, vitu vingi nataka kuviweka sawa, sasa ishu kama hii inaleta mkanganyiko fulani, lakini muda wangu mimi radar uliisha, natakiwa kufanya vitu vyangu vingine", alisema Bill Nas.

Hivi karibuni Bill Nas aliamua kuachana na Radar entertainment ambayo ipo chini ya TID, bila kutoa taarifa kwa msanii huyo, ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa kufika alipo sasa.