Dunia imekwisha! Ndiyo sentensi pekee inayoweza kukutoka baada ya kusikia kisa cha binti huyu aliyejitambulisha kwa jina la Malkia Said a.k.a Malkies, mwenye umri wa miaka 19, mkazi wa Magomeni jijini Dar ambaye amekiri kujihusisha na vitendo haramu vya usagaji akieleza alivyotembea na wanawake wenzake wasiopungua 40 wakiwemo wake za watu zaidi ya 20 hadi kufikia hatua ya kufumaniwa na kunyolewa nywele.
KABLA YA KUFUNGUKA
Kabla ya kufunguka yote hayo, awali habari zake zilivuma kutoka pande mbalimbali jijini Dar na kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kwamba, mrembo huyo ni hatari kwa wake za watu hivyo wenye ndoa zao wakae chonjo.
Baada ya kuvuma kwa jina hilo la Malkies na sifa zake tajwa hapo juu huku ikidaiwa kuwa alifumaniwa na mke wa mtu ndipo gazeti hili likajipa kibarua cha kumtafuta binti huyo ili kujua mbivu na mbichi za msichana huyo.
HUYU HAPA MALKIES
Akizungumza na waandishi wetu ndani ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar, mapema wiki hii, huku akiwa macho makavu, Malkies alisema kuwa, alianza mchezo huo tangu akiwa mdogo kutokana na hisia za mapenzi zilizokuwa zikimsukuma kwa kasi kujihusisha na kitendo hicho haramu.
“Nilipokuwa mdogo, kuna binamu yangu mara kwa mara alikuwa akinivizia akitaka kunibaka lakini nikawa ninamchenga, sasa baba yangu alipofariki dunia nikiwa darasa la nne ndipo nikapelekwa shule moja ya boarding iliyopo jijini Mwanza.
“Muda mwingi nilikuwa na watoto wa kike wenzangu huku msukumo wa kufanya nao mapenzi ukinitesa.
“Kwa kuwa yule binamu yangu alisababisha niwe na hisia kali za mapenzi, nikawa navumilia. Mwisho, nilihamishiwa shule nyingine ya boarding ipo Kibaha (Pwani).
“Huko kuna siku nikawa naumwa, rafiki yangu Mzanzibari akataka kunichumu shavuni. Ndipo tukajikuta tumeingia kwenye mchezo huo rasmi. Nakumbuka hiyo ilikuwa mwaka 2010,” alisimulia Malkies huku akilengwalengwa na machozi.
ASHTUKIWA SHULENI
Alisema, baada ya hapo ilifikia hatua uongozi wa shule ukajua na kuwaambia ndugu zake, akiwemo mama yake lakini walipuuza kwa kuhisi anasingiziwa.
Alisema kadiri siku zilivyosonga ndivyo alivyokubuhu na kupata uraibu uliomfanya kutotamani kuuacha mchezo huo ambao aliamini ndiyo furaha pekee kwake kwani baada ya muda, mama yake naye alifariki dunia.
AJARIBU KUWA NA WANAUME
Alidai kuwa, kutokana na maneno ya kila kukicha watu wakimkemea juu ya ishu hiyo, Malkies aliona bora ajaribu kuwa na mwanaume labda anaweza kuacha, lakini kila mwanaume aliyekuwa naye ambao wanaweza kufikia ishirini, hakuwa akihisi msisimko kama anapokuwa na wanawake wenzake.
“Pia mjomba wangu alikuwa akinikuta na wanaume, ananipiga kwa sababu aliona umri wangu hauruhusu na hakujua kwa nini nafanya hivyo maana nilishindwa kumwambia,” alisema Malkies mwenye umri mdogo lakini aliyepitia mambo mengi ya kikubwa.
AFUMANIWA
Akiendelea kusimulia, Malkies alisema, kwa kuwa anajitambua na anajua nini anachokifanya, alidhani ni vyema kutoka na watu waliomzidi umri kuliko kuwapotosha vijana wa rika lake, ndipo akampata mke wa mtu.
Alisema kabla ya hapo alishakuwa na wake wengine wa watu lakini huyo wa Magomeni hali ilikuwa mbaya kiasi cha kutwangwa talaka na mumewe.
“Nimeshakuwa na wake za watu zaidi ya ishirini, wengi wamenizidi umri pia wake za watu wananitaka wenyewe, huyo mmoja alikuwa anaishi Magomeni na mumewe akawa ananishumbua kwa kipindi kirefu wakati mimi nilikuwa na mtu wangu.
“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoachana na huyo mtu wangu (mwanamke mwenzake), niliamua kuwa na huyo mwanamke.
“Yeye ana umri wa miaka 30, alinidanganya anaishi na baba yake, akanipeleka hadi kwake. Baadaye aliniweka wazi kuwa anakaa na mumewe na majirani wakamfikishia habari mume wake kuwa huwa nakwenda pale akiwa hayupo.
“Kulitokea ugomvi mkubwa kati ya yule mwanamke na mumewe, yule mwanamke akadai talaka na akapewa kwa sababu yangu.
“Niliendelea naye hata baada ya mumewe kumuacha, tukawa tunaishi wote Ubungo kwa dada yake na mimi nikiwa na mtu najiachia kimahaba siwezi kuficha.
“Wiki mbili baadaye, yule dada’ke alichukia, akaita ndugu zake na yule mume, wakaja kunifumania, wakanipiga na kuninyoa nywele.
“Tuliendelea kidogo lakini sasa tumeachana kabisa,” aliongeza binti huyo ambaye pia aliwahi kushiriki kwenye filamu na muziki japokuwa hakuwika.
STAA ANAYEMZIMIKIA
Akiendelea kueleza kwa kujiamini, Malkies alisema, wanawake wengi ambao alikuwa akiwazimia ni Wazungu na chotara, lakini mbali na hao alikuwa akiumiza kichwa na staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kumtunza Sh. milioni moja kwenye shoo huko Arusha.
“Hakuna msanii anayenivutia zaidi ya Wema na siku ile nilipomtunza ni kwa sababu tu alikuwa amelewa na mimi nililewa, lakini tungekuwa sawa ningemueleza jinsi ninavyomkubali,” alisema.
LENGO LA KUJITANGAZA
Alimalizia kuwa, suala hilo siyo jambo la kufumbia macho kwa sababu linafanywa na wanawake wengi wakiwemo mastaa na wake za watu hivyo ameamua kuanzisha shirika la kuwasaidia wengine ambao bado hawajajiingiza na waliojiingiza kwenye vitendo hivyo ili waache kwa lengo la kuokoa kizazi hiki na kijacho