Ni headlines za msanii Flora Mvungi ambae leo October 19, 2016 amefunguka na kutaja kashfa ambayo hatoweza kuisahau maisha mwake.
Mimi sio mgeni macho mwa watu na wengi wananifahamu tabia yangu ikoje na wengi wanafahamu page yangu ya instagram ikoje na sijawahi kumtukana mtu bila sababu ya msingi kitu kikubwa’
‘Kikubwa ni kwamba ilivyotokea taarifa kwamba mimi ndio mmiliki wa ukurasa wa instagram uitwao Marashi ya pemba iliniumiza sana na kuniharibia hata kwa watu wengi ninaowaheshimu kwahiyo ningekupenda kuwaambia mashabiki wangu kwamba zile taarifa za mimi kumiliki huo ukurasa sio za kweli’