Prof. Ndalichako awatupia lawama Bodi ya Mikopo kufanya kazi kwa mazoea, arejesha posho ya 8,500 - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Oct 2016

Prof. Ndalichako awatupia lawama Bodi ya Mikopo kufanya kazi kwa mazoea, arejesha posho ya 8,500

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof. Ndalichako amewatupia lawama bodi ya mkopo elimu ya juu kuwa wanafanya kazi kwa mazoea. Amesema pamoja na kutumia jitiada za kusafisha watumishi bodi hiyo amesema wapo watumishi bado wanafanya kazi kwa mazoea.

Prof. Ndalichako amesema ameyasikia malalamiko kutoka kwa wananchi na anayafanyia kazi na amesema wanafunzi wapewe mikopo semista hii kwa mwaka wa kwanza na wote bila kufuata mean tested.

Amesema lengo la serikali ni kuwapa wote wahitaji. Ameiagiza bodi ya mikopo kuwapa kama mfumo wa zamani na amesema bodi ya mkopo imekosea kuwapa wanafunzi shilingi elfu tano kwa miezi, kama pesa za kujikimu amesema bora kutompa.