"Nilianza U-dj nikiwa na miaka 12" - Dj D'Ommy. - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Oct 2016

"Nilianza U-dj nikiwa na miaka 12" - Dj D'Ommy.


Utoaji wa tuzo za AFRIMMA kwa mwaka 2016 ulifanyika Dallas, Marekani huku watanzania watatu,Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D Ommy wakiibuka na tuzo kila mmoja

Diamond aliondoka na  tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume kwa Afrika Mashariki, Harmonize akishinda tuzo ya msanii anayechipukia Afrika na DJ D Ommy akishinda tuzo ya DJ bora Afrika.
Kwa Upande wa Dj D'Ommy,hii ni mara ya kwanza kwa Dj kutoka Tanzania kushinda tuzo katika fani hiyo nnje ya nchi na hii ndiyo sababu iliyopelekea kumtafuta ili kujua mambo machache kwenye safari yake ya mafanikio aliyofikia,Haya ni baadhi ya mambo usiyoyajua kuhusu Dj D Ommy ambae huwa anasikika kupitia vituo vya Clouds Fm na Clouds Tv;
1.Alianza U-dj akiwa na miaka 12,baada ya kuhamasishwa na Mtangazaji mkongwe nchini,Taji Liundi alipokutana nae enzi hizo Taji Liundi akifanya kazi kwenye kituo chaChanel ten tv.

2.Show yake ya kwanza kufanya kama Dj ilikua mwaka 2012 kwenye Ukumbi wa Mlimani 
City,Dar es salaam,anasema alikua na hofu ila alipata mapokezi mazuri.
3.Anaamini Dj ni kiungo bora kwenye ukuaji wa muziki endapo watu wakiwa wabunifu.
 Image result for Dj D ommy
4.Anasema tuzo yake inamanisha kuwa sasa watu kutoka mataifa mengine watakua wakitazama na kusikiliza anacheza wimbo gani,hivyo ni nafasi ya kuutangaza muziki wa nyumbani kupitia fani yake.
5.Anasema ili mtu awe Dj bora na afanikiwe,anatakiwa kuwa mbunifu,awe tayari kuwekeza,awe  tayari kujitoa kama kuonesha kazi zako mitandaoni hata kama haazitakulipa kwa wakati huo,ikiwa ni pamoja na kumcha Mungu.

6.Baadhi ya Ma-Dj anaowakubali ni pamoja na Dj John Dilinga 'JD',Boni Love,Piter Moo,Stive B na wengine wengi.

Orodha kamili ya washindi ilikua kama ifuatavyo;

Best Male West Africa – Olamide (Nigeria)

Best Female West Africa – Efya

Best Male North Africa – Amr Diab

Best Female North Africa – Ibtissam

Best African DJ USA – Dj Dee Money

Best Male Central Africa – C4 Pedro

AFRIMMA Video of the year – Brother brother Bisa Kdei

Best Female Central Africa – Daphne

Music Producer of the year – Masterkraft

Best male South Africa – AKA

Best Female Southern Africa – Chikune

Best Rap Act – Phyno (Nigeria)

Best African Group – Sauti Sol (Kenya)

Best collaboration – Reggae blues ( Harrysong, Kcee) Nigeria

Crossing boundaries with Music – Wizkid (Nigeria)

Song of the year – Tecno Duro (Nigeria)

Best Gospel Act – Willy Paul (Kenya)

Best Male East Africa – Diamond Platnumz ( Tanzania)

Artist of the year – Flavour ( Nigeria)

Best Newcomer – Harmonize (Tanzania)

Best Dancehall Act – Shatta Wale

Best Video Director – Patrick Elis

Carribean Artist of the year – Machel Montano