Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameamua kutoa ya moyoni kufuatia hali iliyojitokeza jana mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto. Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema kuwa eneo la hospitali hiyo lilitolewa na familia ya Nyaga Mawalla, jambo ambalo wananchi walilipinga wakishirikiana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kuzua sintofahamu kama inavyoonekana katika video hii….
Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook ameandika hivi;
Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook ameandika hivi;
“Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa Mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. Kaa Na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja.Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.”