Mahakama Yamfutia Shtaka la Unyang’anyi wa Kutumia Silaha Scorpion - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Oct 2016

Mahakama Yamfutia Shtaka la Unyang’anyi wa Kutumia Silaha Scorpion

Mahakama ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam leo imemfutia shtaka la  unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete maarufu kwa jina la Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani hapo kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani anatuhumiwa kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa Mabibo Hostel hivi karibuni.