Bilionea huyo alibainisha hayo kwenye mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes kinachorushwa na kituo cha CBS News na kusisitiza msimamo wake wa kutopokea kiasi cha $400,000,fedha anazolipwa Rais wa taifa hilo lenye nguvu na ushawishi ulimwenguni.
Ingawa hakujua Rais hulipwa kiasi gani cha fedha,Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua dola moja pekee ($1) kwa mwaka kama mshahara wake.
Bw Trump si kiongozi wa kwanza wa Marekani kukataa mshahara.Herbert Hoover alikua tajiri kupitia biashara ya madini kabla ya kuingia madarakani kama ilivyokua kwa John F Kennedy, aliyerithi utajiri mwingi kwenye familia yake ambapo wote hawa walikataa kupokea mashahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie wasiojiweza katika jamii.
Aliewahi kuwa Rais wa Marekani,John F.Kenedy.
Si hao tu,hata Meya wa zamani Michael Bloomberg, gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger na gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney pia walikataa kupokea mishahara yao.
Mark Zuckerberg, mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ndiye mfanyakazi anayelipwa mshahara wa chini zaidi katika kampuni hiyo.
Maafisa watendaji wa mtandao wa Google,Sergey Brin na Larry Page pia wamekuwa wakilipwa $1 kwa mwongo mmoja sasa.