Baada ya Ommy Dimpoz kumtuhumu wazi wazi Nassibu Abduli kuwa ana nunua views na tunzo bila kuwa na uthibitisho na bila aibu Ommy ili kuwathibitishia watu kuwa kuwa watu hununua views alisema kuwa hata yeye aliwai kutaka kununua...
Lakini kabla ya hayo tuhuma hizo dhidi ya Nasibu Abduli zilikuwa zinatolewa kwa uwoga na msanii Ali salehe lakini wengi wafatiliaji walikuwa wanaelewa kuwa anaye tuhumiwa ni Nasibu Abduli..
Wanasema uongo ukiongelewa sana bila kukanushwa au kutolewa ufafanuzi hugeuka kuwa ukweli na wale wsiojua ndio huamini kabisa ni kweli.
Leo Clouds Fm waliamua kumtafuta muwakilishi wa You tube East Africa kumuuliza kama kweli watu wanaweza kununua views au viewers na wao wasigundue na kuchukua hatua..
Kwanza Mwakilishi yule aliweka wazi kabisa wao hapa East Afrika wanasimamia na ku control you tube channel za wasanii baadhi East Africa na kwa Tanzania wanasimamia Channel za kina AY,Mwana FA, wasanii wa wasafi wote na Alikiba.
Mwakilishi huyo aliendelea kufafanua kuwa ni vigumu mtu kununua viewers you tube na wasigundue na kuwaondoa na akaendelea kusema You tube ina wataalam wabobezi sana na wanajua kuna watu wanaweza fanya hivyo na hivyo wamejidhatiti sana kimfumo.
Aliendelea kusema kuwa kama ukinunua views wanafungia account yako na hutoweza kufungua account yeyote ile google na gmail account wanaifunga na alisema kuwa kamwe hawawezi kumruhusu mtu kununua views halafu waje kumlipa na haiwezekani.
Alipo ulizwa kuhusu Diamond kununua views alisema hakuna kitu kama hicho na hawewezi kuruhusu mtu anunue views halafu waje kumlipa na kamwe hawatoruhusu hilo hivyo habari hizo si kweli.
Hivyo mwakilishi wa You tube amehitimisha tuhuma na kufunga mjadala mzima juu ya ununuaji wa viewers na ni wazi habari zimemuumbua Ommy Dimpoz
Ommy anapashwa kujitokeza hadharani nakumuomba radhi Bwana Nasibu Addul.