Mwanafunzi mmoja Allie Dowdl (18) amechangisha zaidi ya dola 10,000 kupitia mchango wa raia baada ya kudai kwamba wazazi wake walikata uhusiano na yeye kwa kuwa na mpenzi ambaye ni mweusi aliyetambulika kwa jina la Michael Swift.

Allie Dowdle amesema wazazi wake walikataa kumpatia fedha kwa sababu hawakupenda uhusiano wake na kijana huyo mweusi.

Baba’ke msichana huyo hata hivyo amekana kwamba sababu ya kukata uhusiano huo ni ile ya ubaguzi wa rangi.

Anadai kwamba baada ya mkutano huo wazazi wake walimtenga na sasa hawezi kupata fedha alizohifadhiwa, gari, simu na hawezi kulipia masomo yake.

”Sitasahau vile wazazi wangu walivyonikaripia walipoelezea vile walivyokasirishwa nami kwamba ningeweza kutafuta mtu