Breaking Newss... Rais Magufuli Amvua Ubunge na Uwaziri Dkt. Possi, Ampa Ubalozi - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Jan 2017

Breaking Newss... Rais Magufuli Amvua Ubunge na Uwaziri Dkt. Possi, Ampa Ubalozi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 19 Januari, 2017 amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi.
 
Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Dkt. Abdallah Possi itatangazwa baadaye.
 
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah Possi alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.
 
Kufuatia uteuzi wa Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi, nafasi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu (Ulemavu) itajazwa baadaye.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam