Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Solo Thang amefunguka baada ya baadhi ya watu kumjia juu kwa kusambaza kipande cha video alichorekedi akiwa na Chidi Benz.
Akiongea kwenye kipindi cha E News cha EATV, Solo amesema kuwa Chidi ndiye aliyemtaka amshoot video wakati walipokutana ila hakuwa na nia kama watu wengine wanavyofikiria.
“Chidi ni mdogo wa rafiki yangu na nilimfahamu zamani sana kabla hata hajaanza kuimba. Hivyo tuna historia ndefu kidogo. Chid kwa sasa huwa hapigi picha na watu, lakini tulipoonana ni yeye mwenyewe ndiye alitaka tushoot ile video lakini sikuwa na nia ya kumchoresha,” amesema Solo.
Rapper huyo ameongeza kuwa watu waache kumlaumu Chidi kwa kile kilichomtokea na badala yake wanatakiwa kumpatia msaada bila ya kuchoka.